MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa, amesema mapato yaliyokusanywa na TPA kwa kipindi cha Julai, 2023 hadi Juni, 2024, yamefikia Sh. trilioni 1.4.
Amesema, kulingana na taarifa mbalimbali za kiuchumi, mchango wa sekta ya Bandari katika mapato yanayokusanywa na TRA, umeendelea kuwa kati ya asilimia 38 hadi 40 ya mapato yote yanayokusanywa.
Aidha, alisema kwa mujibu wa taarifa za TRA, mapato yatokanayo na ushuru wa forodha yameongezeka kwa asilimia 18 kutoka wastani wa Sh. bilioni 850 kwa mwezi hadi kufikia wastani wa Shilingi Trilioni 1.
“Pamoja na sekta ya Bandari kuchangia katika mapato ya nchi, sekta hii huchangia katika kutoa ajira za moja kwa moja kwa kuwa, taasisi za umma na binafsi zinazofanya kazi bandarini, zimeajiri watumishi wanao toa huduma bandarini.
“Kwa mfano, kwa siku magari yanayoshushwa na kutolewa nje ya Bandari ya Dar es Salaam, ni wastani wa magari 600 na wastani wa magari ya kubeba mizigo 1,500 huingia kupakia na kushusha shehena bandarini, sawa na wastani wa ajira za madereva 1,600 kila siku,” alisema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED