SERIKALI kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imesema itatekeleza miradi 10 ya kimkakati, ukiwamo mradi wa kupokelea na kuhifadhi mafuta SRT.
Imesema utekelezaji wake umefikia asilimia 17 na unagharimu dola za kimarekani million 265.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa, alisema hayo jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya mamlaka hiyo katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita.
Alisema, mradi huo ukikamilika utapunguza siku za kuhudumia meli zenye ujazo wa 150,000 DWT kutoka siku 10, mpaka tatu.
Alisema mradi mwingine ni uendelezaji wa bandari kavu eneo la kurasini (Kurasini Logistics Centre) na Ihumwa–Dodoma, ambayo itagharimu dola za kimarekani million 157, unaolenga kuongeza maeneo ya kufanyia shughuli za utekelezaji, uchakataji na kuhifadhi shehena kwa muda.
“Ujenzi wa kituo cha reli na mtandao wake ndani ya bandari ya Dar es Salaam na unagharimu dola za kimarekani million 119.955.
“Mradi huu ukikamilika utapunguza kiwango cha asilimia 98 cha shehena, inayotoka bandarini kwa kutumia njia ya barabara na kupelekea kutatua tatizo la msongamano wa malori ndani na nje ya bandari,” alisema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED