RAMADHANI; Rais Mwinyi aagiza w’biashara kuepuka bei juu

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:34 PM Feb 24 2025
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi
Picha: Mtandao
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameeleza kuridhishwa na upatikanaji wa bidhaa za vyakula na kuwataka wafanyabiashara kutopandisha bei wakati Ramadhani itakapoanza.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo alipotembelea asoko ya Jumbi, Mwanakwerekwe na Darajani, kuangalia mwenendo wa biashara  na upatikanaji wa bidhaa za vyakula  kuelekea mwezi wa Ramadhani.

Aidha Rais Dk. Mwinyi,  ameeleza kuwa serikali inajipanga, kwa ajili ya ujenzi wa masoko mengine maeneo mbalimbali, ili kila mfanyabiashara afanye biashara  kwenye mazingira  rasmi.

kuhusu suala la  usafi wa masoko ameuagiza uongozi wa masoko hayo, kutafuta njia bora zaidi ya uhifadhi wa bidhaa za wafanyabiashara, ili kuwa safi wakati wote.

Amezielekeza taasisi zinazosimamia masoko hayo kuhakikisha upatikanaji wa  huduma ya maji na vipooza hewa katika masoko yote, pamoja  na kuimarisha usafi.

Ziara hiyo ya Rais Dk. Mwinyi ni ya wanza tangu kufunguliwa kwa masoko hayo na ukarabati mkubwa wa soko la darajani.