PAPA Francis, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, bado yupo katika hali inayoelezwa ni mbaya, baada ya kubainika ana tatizo la figo.
"Hazijaonyesha dalili za ziada za matatizo ya kupumua," ilisema Vatican katika taarifa iliyotolewa jana, Jumapili.
Papa alikuwa bado akitumia mipira ya oksijeni yenye mtiririko mkubwa na alikuwa amewekewa damu.
Vipimo vya damu pia vilionesha kwamba alikuwa na changamoto ya awali ndogo ya tatizo la figo, ambalo kwa sasa linaweza kudhibitiwa, kwa mujibu wa taarifa hiyo.
Vatican ilisema kwamba "anaendelea kuwa mwenye kujielewa na mwenye ufahamu mzuri."
Papa alifikishwa katika hospitali ya Gemelli, huko Roma, Italia, Februari 14, mwaka huu, baada ya kupata shida za kupumua kwa siku kadhaa.
Alihudumiwa kwanza tatizo hilo, kabla ya kugundulika kuwa ana homa ya mapafu iliyoathiri mapafu yake yote mawili.
Pamoja na hali yake hiyo, Jumapili asubuhi, Papa "alishiriki katika Misa Takatifu pamoja na wahudumu wanamuhudumia Hspitalini hapo," iliongeza taarifa hiyo.
Taarifa hii mpya inafuata taarifa ya Jumamosi, Vatican ilisema kwamba Papa alikuwa ameonekana tatizo kwenye mapafu yake na kutatiza upumuaji wake na alikuwa katika hali "mbaya sana."
Awali Jumapili, Papa alitoa taarifa akiomba waumini wa Kanisa Katoliki kumuombea, baada ya kushindwa kuungana na waumini wa kanisa hilo, kwenye ibada ya jadi ya kila jumapili kwa wiki ya pili mfululizo.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki la Roma, amekuwa akihudumiwa hospitalini mara kadhaa, wakati wa utawala wake wa miaka 12, ikiwa ni pamoja na matibabu ya Machi 2023.
Akitokea Argentina, Papa Francis (88) ni wa kwanza kutoka bara la Latin Amerika na wa kwanza kutoka Jesuit, kuongoza Kanisa Katoliki la Roma.
BBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED