MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, ikiwamo kumwombea kura Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, katika uchaguzi mkuu 2025.
Amesema wakazi wa maeneo hayo wampigie kura nyingi za ushindi, huku akijieleza kwa wananchi yale aliyoyatekeleza ndani ubunge, chini ya Rais Dk. Samia.
Katambi, ameanza ziara hiyo jana, kwa kuzungumza kwanza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Kata ya Kizumbi na Ibinzamata, kwenye vikao vya ndani na kisha kufanya mkutano wa hadhara.
Katika mkutano huo amewaeleza wananchi kuwa, ndani ya miaka minne ya ubunge, ameibadilisha Shinyanga kimaendeleo na ahadi nyingi ambazo aliahidi amezitekeleza, huku akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kumshika mkono kwa kila anachokiomba.
Ametaja miradi ambayo ameitekeleza kila sekta, upande wa elimu kipindi anaingia kwenye ubunge Shinyanga Mjini, kulikuwa na shule 65 za Msingi na sekondari, lakini wamejenga shule mpya 10 mpya.
Akisema hadid sasa wamefikisha shule 75, pamoja na kujengwa pia shule ya wasichana, ambayo haikuwapo, huku wakitatua pia tatizo la upungufu wa walimu kutoka 421 hadi 180.
Amesema pia wanapanua Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Tawi la Kizumbi, zimepatikana kiasi cha fedha Sh. bilioni 11 kwa ajili ya kuongeza majengo, ili kiwe na wanafunzi 3,000 pamoja na kuwapo na mikakati ya kupanua Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto na pia wameleta Tawi la Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, kuongeza mzunguko wa fedha.
Kwa upande wa miundombinu ya barabara, ametatua changamoto kwenye maeneo ambayo yalikuwa korofi, pamoja na kujenga madaraja, huku akimpongeza Rais Samia kuendelea kutoa fedha za ujenzi wa barabara, ikiwamo na Barabara ya kwenda Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Shinyanga-Mwanza kwa kiwango cha lami.
Kwa upande wa huduma ya maji, amesema maeneo mengi yamefikiwa na huduma hiyo na kwamba kuna fedha imepatikana Sh. bilioni 195 zipo SHUWASA, kwa ajili ya kusambaza zaidi mtandao wa maji kwa wananchi.
“Kazi ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya kumtua ndoo kichwani mwanamke ipo pale pale, ndiyo maana anatoa fedha na miradi mingi ya maji inazidi kutekelezwa, Mama ukimuomba anasikia na kutekeleza,” amesema Katambi.
Amegusia pia suala la afya kwamba ndani ya ubunge zimeimarika zaidi, ikiwamo ujenzi wa zahanati, vituo vya afya, upatikanaji wa vifaatiba na dawa pamoja na ukarabati wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga na ya Mkoa.
Pia, amewasihi vijana kuchangakia fursa ya masomo bure ya kupata ujuzi ambayo inafadhiliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa kusoma bure katika Chuo cha Hillforest cha Shinyanga, ambapo wataweza kujiajiri na kuendesha maisha yao.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Hamisa Chacha, amempongeza Mbunge, kwa kuitendea haki ilani ya uchaguzi ya chama hicho, ahadi ambazo aliwaahidi wananchi, amezitekeleza.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga, Dk. Elisha Robert, akijibu swali la ukamilishaji wa zahanati amesema kwanza anamshukuru Rais Samia, pamoja na Mbunge Katambi, sababu manispaa hiyo kuwa na Maboma 16, lakini sita yamekamilishwa na yanatoa huduma, huku mbili ya Mwagala na Mwamagunguli, yapo hatua za mwisho za ukamilishaji.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED