Wafanyakazi taasisi ya OYA kizimbani tuhuma za mauaji

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:06 PM Oct 16 2024
Wafanyakazi taasisi ya OYA kizimbani tuhuma za mauaji.

WAFANYAKAZI wanne wa Taasisi ya mikopo ya OYA, leo Oktoba 16,2024 wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kibaha kwa madai ya kumuua Mkazi wa Kitongoji cha Mbagala Mlandizi mkoani Pwani, Juma Said (45).

Wafanyakazi taasisi ya OYA wakiwa katika viunga vya mahakama leo.
Watuhumiwa hao ni Emmanuel Olla (24), Dastan Charles (23), Christopher Charles (23) wakazi wa Kilangalanga Mlandizi, na Abdallah Wendiliwe (32) mkazi wa Janga Mlandizi mkoani humo.

Mara baada ya kusomewa mashtaka yao, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Emmanuel Lukumai amesema udhahidi wa kesi hiyo haujakamilika na kuihairisha hadi Oktoba 30, 2024 huku watuhumiwa wote wakirudishwa rumande.

Tukio hilo lilitokea Oktoba 9, 2024, baada ya vijana hao kufika nyumbani kwa mdaiwa ambaye ni mke wa Juma kisha kumshambulia mumewe hadi akapoteza maisha.