Prof. Janabi aonya huduma ya 'massage' kwa wenye kiharusi

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 06:38 PM Oct 16 2024
MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)-Mloganzila, Prof. Mohamed Janabi
Picha: Christina Mwakangale
MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)-Mloganzila, Prof. Mohamed Janabi

MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Mohamed Janabi ametahadharisha jamii huduma ya 'massage' kwa waougua kiharusi, akisema huduma pekee ya kitabibu ni kumfanyia mgonjwa fiziotherapi.

Amesema huduma hiyo ya 'massage' haimpi nafuu mgonjwa, badala yake humuongezea ulegevu wa mwili na misuli na kushindwa kuimarika.

Prof. Janabi, ameyasema hayo leo, Dar es Salaam, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ongezeko la ugonjwa huo.

Amesema kwa miaka miwili kwa upande wa wagonjwa wa nje (OPD) idadi imeongezeka kuanzia Oktoba 2022 hadi Septemba 2024 katika Kliniki ya Ubongo na Mishipa ya Fahamu,  wamehudumiwa wagonjwa 10,271 huku wagonjwa wa ndani (waliolazwa) wakiwa ni wastani wa wagonjwa 2,953.