Umoja wa wanafunzi waliosoma Milambo wazindua tuzo ya Mwalimu Bora

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 04:25 PM Oct 12 2024
Umoja wa wanafunzi waliosoma Milambo wazindua tuzo ya Mwalimu Bora.
Picha: Mpigapicha Wetu
Umoja wa wanafunzi waliosoma Milambo wazindua tuzo ya Mwalimu Bora.

Umoja wa wanafunzi waliosoma shule ya sekondari Milambo, iliyoko mkoani Tabora wamezindua zawadi ya Mwalimu Bora wa Mwaka kwa shule hiyo.

Uzinduzi huo umefanyika kijijini Mwitongo, Butiama mkoani Mara alikozaliwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa umoja huo, Abdul-Razak Badru,  mshindi wa tuzo hiyo atakua akipewa zawadi na fedha taslimu.

Aidha, zawadi ya kwanza ya mwalimu bora  kwa heshima  imeenda kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambae aliwahi kufundisha shule hiyo ya Milambo wakati huo ikiiitwa St Merrys.

Zawadi hiyo imepokelewa na mtoto wa Mwalimu Nyerere, Madaraka Nyerere kwaniaba ya familia.