Ndolezi aanza ziara Kigoma

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 04:00 PM Oct 12 2024
WAZIRI Kivuli ACT Wazalendo Ofisi ya Waziri Mkuu -Bunge Sera Vijana Kazi na Ajira Mhandisi Ndolezi Petro.
Picha: Mpigapicha Wetu
WAZIRI Kivuli ACT Wazalendo Ofisi ya Waziri Mkuu -Bunge Sera Vijana Kazi na Ajira Mhandisi Ndolezi Petro.

WAZIRI Kivuli ACT Wazalendo Ofisi ya Waziri Mkuu -Bunge Sera Vijana Kazi na Ajira Mhandisi Ndolezi Petro ameanza ziara yake Katika Jimbo la Kigoma Kusini ya kuzifikia Kata 16 na Vijiji 61.

Kwenye Kikao alichofanya na Kamati ya uongozi ya Jimbo hilo jana tarehe 11 amewakabidhi vitendea kazi viongozi wa Jimbo vitavyoweza kusaidia wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. 

Vitendea kazi hivyo ni pamoja na Mihuri ya Makatibu Tawi kwenye Vijiji vyote 61 na Kata 16,  amekabidhi pia Stamp Pad 72 za wino wa Mihuri, Bendera 32 , Vipeperushi 300 vya ratiba ya uchaguzi.

Vifaa vyote hivyo vimepokelewa na Viongozi wa Jimbo la Kigoma Kusini wakiongozwa na Katibu wa Jimbo hilo, Yakubu Nzigamiye ambao watavishusha kwa viongozi wa Kata na Matawi.

Ndolezi pia amewataka viongozi waendelee kufanya kazi ya kuhamasisha Wanachama wa Jimbo hilo kujiandikisha na kuhakikisha wagombea wenye sifa na kukubalika wanapata nafasi ya kugombea na kuweza kupata fursa ya kuwatumikia Wananchi.

Vilevile alitoa wito kwa Wananchi wa Jimbo la Kigoma Kusini kujitokeza kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Kila akisisitiza kila mwenye sifa ya kuchagua ajiandikishe.