Ukishindwa kuhimili hisia zako, chanzo magonjwa ya akili

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 07:01 PM Oct 18 2024
Dk. Nuruel Kitomary.
PICHA: CHRISTINA MWAKANGALE
Dk. Nuruel Kitomary.

UWEZO duni wa kuhimili hisia kunatajwa kusababisha changamoto, matatizo na magonjwa ya akili.

Anasema Bingwa wa Afya na Magonjwa ya Akili kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Nuruel Kitomary.

Anasema kushindwa kuzikabili hisia husababisha  mtu kuwa na mtazamo hasi na kusababisha hasira.

“Usahaulifu usio wa kawaida, kulipuka kwa hasira, kuumwa mgongo ni tatizo na ukifanya vipimo vitu vyote sawa, inaweza kuwa dalili ya sonona.

Afya ya akili ni utimamu wako ukiwa na utengamao kijamii, kiuchumi na kielimu, kimahusiano.

Pia ni hali ya kuhimili na kuwa na uwezo wa kufanya kazi na kuizalisha ikaonekana na yenye matunda.

Mtu mwenye uwezo wa kushiriki shughuli za kijamii kiimani, kiuchumi ni utengamao wa afya ya akili,” anasema.

Bingwa huyo anatoa elimu hiyo leo, akizungumza na Chama cha Waandishi wa Habari kuhusu Afya ya Akili Tanzania (TAMHJO) mada: Afya ya Akili Mahali pa Kazi.

Anasema kuwa mwezi huu ni maalumu kukuza uelewa kuhusu afya ya akili.

“Mtu kuutambua uwezo wake binafsi na kukabili changamoto za maisha yaani msongo wa kila siku, utokanao na sababu za asili au za kibinadamu, ndio utimamu.

Wasiwasi, kiwewe, sonona, kukosa usingizi ni kati ya dalili za magonjwa ya akili amabyo yanafikia 200. 

Mara nyingi inahitaji namna ya kuzikabili hisia zako dhidi ya tukio lililoko mbele yako, liwe hasi au chanya,” anasema.

Hatua zote za maisha kuanzia ujauzito unahitaji kumuweka mama sawa kiakili. 

Utakuta mtu ana huzuni muda wote, uso uko ‘flat’ muda wote inaweza kuwa dalili za anajitenga, hacheki. magonjwa ya akili.”