MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge, amefanya ukaguzi wa mabanda ya maonyesho ya biashara za viwandani yanayoanza leo mjini Kibaha, yakiwemo mabanda ya Kampuni ya Kinglion.
Maonyesho hayo, yanayofanyika kwa mara ya nne sasa, yamewaleta pamoja wawekezaji mbalimbali kutoka mkoani humo kwa lengo la kuonyesha bidhaa zinazozalishwa ndani ya Mkoa wa Pwani.
Kampuni ya Kinglion ni miongoni mwa washiriki wa maonyesho hayo, ikionyesha bidhaa zake kama pikipiki za mizigo (guta) zinazotumia mafuta na umeme. Akizungumza katika maonyesho hayo, Afisa Mauzo wa kampuni hiyo, Asha Idd, alisema maonyesho haya yanawapa wananchi fursa ya kujionea bidhaa mbalimbali na kujifunza namna ya kuzipata.
“Mbali na pikipiki za mizigo, tunatoa pia malighafi za kuzalisha mabati ambazo zitakuwepo katika maonyesho,” alisema Asha.
Kampuni ya Kinglion inamiliki viwanda katika mikoa mitano nchini, ikiwemo Dodoma, Mwanza, Arusha, Mbeya, na Zanzibar, na imeendelea kuchangia ukuaji wa sekta ya viwanda nchini.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED