Kamati Kuu CHADEMA yateua wagombea viti vya kina Lema

By Elizabeth Zaya , Nipashe
Published at 12:58 PM Dec 16 2024
Kamati Kuu CHADEMA yateua wagombea viti vya kina Lema
Picha:CHADEMA
Kamati Kuu CHADEMA yateua wagombea viti vya kina Lema

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeteua wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kwa kanda mbili.

Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema si miongoni mwa wagombea wa nafasi hiyo kwa kanda hiyo. 

Lema alishatangaza siku nyingi kuwa hatogombea katika nafasi hiyo huku jina lake likiwa miongoni mwa yanayotajwa huenda yakawamo katika orodha ya wanaotaka kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema, uteuzi wa wagombea uongozi kwa Kanda ya Kaskazini na ya Kati, umefanywa na Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi Desemba 14 mwaka huu.

Wagombea walioteuliwa ni kwa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Mtunza Hazina Kanda na mabaraza.

Kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini aliyeteuliwa ni Antony Mallya, Michael Kilawila na Samweli Welwel.

Kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti, walioteuliwa ni Gervas Sulle, Elifuraha Matela na Emmanuel Landey. 

Walioteuliwa kwa nafasi ya Mhazini ni Bahati Mollel na Emma Kimambo.

Kwa upande wa Baraza la Wazee, wanaogombea nafasi ya Uenyekiti ni Kidawa Iyavu na Leonard Mao wakati nafasi ya Makamu Mwenyekiti inawaniwa na mgombea mmoja, Jomba Koyi na nafasi ya Katibu wa Baraza hilo, aliyepitishwa ni Julius Sarmet.

Walioteuliwa Baraza la Wanawake kwa nafasi ya Uenyekiti ni Luisesia Ndesamburo, Makamu Mwenyekiti ni Rebeca Mngodo wakati nafasi ya Katibu ni Rachel Kiogwe, Jackline Kimabo na Mamuu Lolo na nafasi ya Mhanzini ni Zuena Mwanga.

Upande wa Baraza la Vijana, nafasi ya Uenyekiti wanaogombea ni Gasper Temba na Jakson Msoka, wakati nafasi ya Katibu ni Amani Kimath na Beda Fransis. 

KANDA YA KATI
Kwa Kanda ya Kati, wanaogombea nafasi ya Uenyekiti Chama ni David Mghanja, Devotha Minja, Ezekiel Chisinjila, Idd Kizota na Shujaa Evarist, wakati nafasi ya Makamu Mwenyekiti wanaogombea ni Daniel Marwa, Godfrey Charles, Imelda Malley na Jingu Jackson na nafasi ya Uhazini, wanaogombea ni Honest Msaki, Kapalatu Singamagazi na Modestus Chitemi.

Upande wa Baraza la Wazee, wanaogombea ni Aquilin Magalambula, Mathew Likwina, wakati nafasi ya Makamu Mwenyekiti wanaogombea ni Ester Jingu, nafasi ya Katibu ni Paul Eugen na nafasi ya Mhazini ni Jella Mambo.

Kwa upande wa Baraza la Vijana la Kanda hiyo ya Kati,  Kamati Kuu imewatea wanaogombea Silvery Dodo na Hilda Mbuli kwa nafasi ya mwenyekiti.