Mianzi kunufaisha vijana 5,000 Kibaha

By Beatrice Moses , Nipashe
Published at 08:13 PM Oct 21 2024
Mianzi.
Picha:Mtandao
Mianzi.

Vijana zaidi ya 5,000 wanatarajiwa kunufaika na kilimo cha mianzi, baada ya Uwekezaji wa miradi wa kilimo hicho kuzinduliwa.

Meya wa Kibaha Mussa Ndomba alisema mradi huo ni neema hasa kwa vijana kwa kuwa itatoa fursa ya kupata ajira, na kujifunza kilimo hicho hivyo nao wanaweza kulima kwenye maeneo hayo hasa wakiwa na uhakika tunza mazingira.  

“Kibaha ni eneo la kiuwekezaji kimsingi nafikiri linaongoza iwe katika kilimo au viwanda Tanzania yote ni eneo la kimkakati, kila unachokusudia kukifanya kuhusu uwekezaji kinawezekana, kwa hiyo tunaendelea kukaribisha wawekezaji,” alisema Meya Ndomba. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shikana Group Amne Kageshi, ambayo ni washauri wa wawekezaji  wa mradi huo Silver Terra alisema katika awamu ya kwanza ya mradi wamekusudia kuwekeza kwenye kilimo hizo dola za Marekani milioni 50 na vijana takribani 5,000 watapata ajira za mikataba

Mkurugenzi wa Silver Terra Carl-Lambert Liesenberg alisema nia yao ni kuungaisha shughuli za kiuandisi ujenzi wa Uswizi na Tanzania, ikimaanisha kwamba wanaweza kuendeleza ujenzi wa majengo kwa miti ya mianzi kwa ujuzi wao wa Uswizi. 

Waziri wa Mipango na uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo mwishoni mwa wiki amezindua mradi  huo wa upandaji wa miti hiyo unaotarajiwa kuanzia Kibaha mkoani Pwani  ambao unatarajia kugharimu takriani Sh.280 bilioni.