China kuifanya Tanzania kuwa kitovu kidijiti

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 06:47 PM Oct 21 2024
China kuifanya Tanzania kuwa kitovu kidijiti.
Picha: Mtandao
China kuifanya Tanzania kuwa kitovu kidijiti.

CHINA inaenda kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha kidijitali katika mawasiliano baada ya mataifa hayo mawili kuingia mkataba wa ushirikiano katika sekta hiyo ambayo pia itachochea uchumi na kuongeza ufanisi wa teknolojia ya mawasiliano.

Mapema leo mkoani Dar es Salaam Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesaini mkataba wa ushirikiano na Kampuni ya Teknolojia ya Mawasiliano ya China (CECIS) ukilenga kuja kuongeza ufanisi katika usalama wa mtandaoni nchini.

Akizingumza wakati wa hafla ya kusaini makubaliano hayo Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Maryprisca Mahundi, amesema mkataba huo pia utasaidia katika kutoa mafunzo kwa watanzania kuhusu masuala mbalimbali ya usalama wa mtandaoni.

Amesema mkataba huo pia utasaidia wajana na watanzania kwa ujumla kuwa na uwezo wa kufungua viwanda vyao wenyewe vitakavyotumika katika kutengeneza vifaa mbalimbali vya kielektroniki vinavyotumika katika mawasiliano kama mfano WiFi.

“Haya yote ni matokeo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoifanya nchini China, ambako moja ya kampuni alizozifikia ni hii tunayoenda kushirikiana nayo, sisi kama wizara tunajivunia na wataalamu wetu kwakua tumehakikisha tunafanya harakla katika mawasiliano ili hawa wenzetu waje kwa wakati.

“Lengo ni kuona kwamba tunakwenda kuzikamata zile fursa kwa haraka sana, na tunajenga ‘habs’ vituo vya tehama nane katika nchi hiitayari fedha zimetoka, kazi zimeanza, na tunauhakika ujuzi walionao hawa wenzetu utaenda kutumika katuika majengo hayo kuhakikisha tunaendelea kiteknolojia,” amesema Maryprisca.

Ameongeza kuwa vijana wa kitanzania watanufaika moja kwa moja kwa kupata elimu kutoka kwa wabobezi hawa wa masuala ya usalama wa mtandaoni, na wanataka wafike mbali zaidi kwa kuwalendea viwanda vinavyotengeneza vifaa ili ifike wakati kusiwe na haja tena ya kuagiza vifaa vya mawasiliano nje pale taifa litakapokuwa na uhitaji.

3