Mavunde azindua magari 25 ya maofisa madini wakazi mikoa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:33 PM Oct 21 2024
Mavunde azindua magari 25 ya maofisa madini wakazi mikoa
Picha: Mpigapicha Wetu
Mavunde azindua magari 25 ya maofisa madini wakazi mikoa

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amezindua magari mapya 25 kwa ajili ya kusambazwa kwenye Ofisi za Maofisa Madini Wakazi wa Mikoa na kuwataka kuhakikisha yanatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Akizungumza kwenye  uzinduzi huo,  Waziri Mavunde amesema magari hayo ni sehemu ya magari 89 na pikipiki 140 yaliyopangwa kununuliwa kama sehemu ya uboreshaji wa  usimamizi wa sekta ya madini kwenye ukusanyaji wa maduhuli na kudhibiti mianya yote ya upotevu wa mapato.

“Kwa kmwaka wa fedha 2024/25 tumepewa lengo la kukusanya kiasi cha Sh. Trilioni Moja ambapo ndani ya siku 90 tumeweza kukusanya kiasi cha sh.bilioni 287 ikiwa ni asilimia 106 ya lengo la kukusanya kiasi cha sh.bilioni 249 ndani ya kipindi husika,” amesisitiza Waziri Mavunde.

Naye, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo amesema sh.Bilioni 18 zimepangwa kununua magari na pikipiki hizo.