Mchengerwa: Umewekwa utaratibu maalumu kudhibiti udanganyifu katika uchaguzi

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 08:35 PM Oct 21 2024
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa.
Picha:Mtandao
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amesema, umewekwa utaratibu maalumu wa kuzuia udanganyifu katika uchaguzi ikiwamo mpiga kura mmoja kupiga zaidi ya mara mbili katika vituo tofauti akisisitiza watatumia mifumo ya kiusalama kubaini.

Mchengerwa ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam, alipofunga zoezi la uandikishaji wapiga kura katika daftari la makazi lililodumu kwa siku 10.

Amesema baada ya kumaliza hatua hiyo, orodha ya wapiga kura itabandikwa katika sehemu za matangazo ya uchaguzi ili kuwawezesha wananchi wahakiki majina yao.

Pia amewataka wananchi wenye sifa za kuchaguliwa kuwa viongozi wajitokeze kuanzia Oktoba 26 mpaka Novemba mosi ili waweze kutimiza haki yao ya kikatiba kugombea katika nafasi za uongozi.