Kampuni ya simu kufikisha manufaa 'intarnet' kwa jamii

By Faustine Feliciane , Nipashe
Published at 08:47 PM Jun 04 2024
Mkuu wa Biashara wa Tigo, Isack Nchunda (Kulia), akijadiliana kitu na Mkuu wa kitengo cha ukuzaji masoko wa kampuni hiyo, Daniel Nnko, jana wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Sako kwa Bako na Energizer jijini Dar es Salaam.
Picha: Mpigapicha Wetu

KAMPUNI ya simu ya Tigo, imeelezea mikakati yake ya kuchochea matumizi ya simu janja ili kuonyesha umuhimu na manufaa ya kutumia 'Internet ' kwa jamii kwa ajili ya kukuza maendeleo.

Hayo yamesema leo na Afisa Mkuu wa Biashara wa kampuni hiyo, Isack Nchunda wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ' Sako kwa bako" na Energizer jijini Dar es Salaam.

Nchunda, alisema kampeni hiyo itasaidia wateja wake kupata simu janja na kuongeza matumizi ya Internet hapa nchini.

" Kwa kufanya hivi, sio tu tunachangia watanzania kufikiwa na huduma za kidigitali kwa wingi zaidi bali pia tunahakikisha wanapata uzoefu mzuri wa kidigitali. Simu hii mpya imetengenezwa kukidhi mahitaji ya wateja wetu huku ikiwa imesheheni sifa lukuki, " alisema Nchunda.