Serikali yaja na teknolojia mpya kutibu selimundu

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:18 PM Feb 06 2025
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel
Picha: Mpigapicha Wetu
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel

SPIKA wa Bunge, Dk.Tulia Ackson, ameridhishwa na majibu ya kitaalamu wa Wizara ya Afya, baada ya Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, kuelezwa kuhusu matumizi ya teknolojia ya CRISPR-Cas9 katika matibabu ya magonjwa ya selimundu.

Dk. Mollel alitoa majibu hayo wakati akjibu swali la nyongeza, lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima. 

Dk. Mollel ameeleza jinsi teknolojia ya CRISPR-Cas9 inavyoweza kufanya uhariri wa jeni (gene editing) kwa usahihi mkubwa, bila kuathiri maeneo mengine ya mwili.

Amebainisha kwamba teknolojia hiyo ni ya kisasa na itakuwa na mchango mkubwa katika kutibu magonjwa ya kurithi, yakiwamo magonjwa ya selimundu. 

Katika swali lake, Gwajima alitaka kujua wizara imejiandaaje kupeleka muswada bungeni, ili kuleta sheria maalum itakayoongoza watu kufanyiwa tiba hiyo.