WANAMGAMBO wa M23 inayotajwa kuungwa mkono na Rwanda leo Februari 6, 2025 wameitisha mkutano wao wa kwanza wa hadhara na wananchi tangu wauteke Mji wa Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Mkutano huu unakuja baada ya mapigano makali, ya wapiganaji wake wanaoelekea katika mji mkuu mwingine wa eneo hilo.
Baada ya kuuteka Goma, mji mkuu katika jimbo la Kivu Kaskazini, wiki iliyopita, kisha kuweka mapumziko wanajeshi wa M23 walianzisha mashambulizi mapya siku ya Jumatano katika jimbo jirani.
Mapigano hayo yanavunja usitishaji mapigano ambao ulikuwa umetangaza kwa upande mmoja. Katika mapigano hayo wapiganaji hao waliuteka mji wa uchimbaji madini wa Kivu Kusini wa Nyabibwe, takriban kilomita 100 (maili 60) kutoka mji mkuu wa kikanda wa Bukavu.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kibinadamu vilivyoengea na Shirika la habari la AFP vilisema siku ya leo Alhamisi kwamba vikosi vya Kongo vilikuwa vikijiandaa kufanya mashambulizi katika mji wa Kavumu, ambao ni mwenyeji wa uwanja wa ndege wa jimbo hilo na uko umbali wa kilomita 30 kutoka Bukavu.
Kadhalika vifaa na wanajeshi wanahamishwa ili kuepusha kukamatwa na kundi la M23 linalosonga mbele na washirika wake wa Rwanda.
Kuanguka kwa Kavumba, kizuizi cha mwisho kabla ya Bukavu, litakuwa ni pigo na kikwazo kingine kikubwa kwa jeshi na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika ukombozi wa maeneo yaliyotwaliwa na M23.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED