MAHAKAMA ya Tanzania, imepokea dola za milioni 90 sawa na Sh. bilioni 230, zitakazotumika katika kukamilisha ujenzi wa mahakama tisa za Haki Jumuishi nchini.
Hatua hiyo ni mafanikio ya kusikilizwa na kumalizika kwa mashauri 2000, kwa mwaka 2024/25 ambayo ni sawa na asilimia 98.5.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Prof. Elisante Ole Gabriel, amesema hayo leo, wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mahakama na majukumu kwa nusu ya mwaka wa fedha 2024/25.
Prof. Ole Gabriel, amesema fedha hizo zimetokana na manufaa yaliyojitokeza wakati wa utekelezaji wa vituo sita vya Haki Jumuishi nchini na kwamba fedha hizo zilizotolewa na Benki ya Dunia (WB),
Akizungumzia utendaji wa vituo hivyo vya mahakama na Haki Jumuishi, Msaidizi wa Mawakili wa Kujitegemea, Ivan Calvin, anasema maboresho hayo ya mahakama kupitia vituo vya Haki Jumuishi na mahakama zinzotembea, yametoa hamasa ya ufanyaji kazi na kuwapo kwa huduma za kidigitali kumeepusha gharama na upatikanaji huduma ni haraka kwao na kwa wananchi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED