Dk. Biteko kushiriki Jukwaa la Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali

By Grace Gurisha , Nipashe
Published at 04:19 PM Aug 27 2024
Mwenyekiti wa Jukwaa Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO), Jasper Makalla akisikiliza maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini DaresSalaam, baada ya kuzungumza kuhusu jukwaa la nne la linatarajia kufanyika jijini Dodoma Septemba 4 hadi Septemba 6
Picha: Grace Gurisha
Mwenyekiti wa Jukwaa Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO), Jasper Makalla akisikiliza maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini DaresSalaam, baada ya kuzungumza kuhusu jukwaa la nne la linatarajia kufanyika jijini Dodoma Septemba 4 hadi Septemba 6

WAZIRI wa Nishati Dk Dotto Biteko anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Jukwaa la Nne la Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali( NaCoNGO), ambalo litakuwa na washiriki zaidi 2,000.

Jukwaa hilo linatarajia kufanyika  Septemba 4 hadi Septemba 6, 2024 jiji Dodoma, ambapo kauli mbinu ya mwaka huu ni“Mashirika Yasiyo ya Kiserikali , ni wadau muhimu, washirikishwe katika kukuza utawala bora” 

Taarifa hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Baraza hilo Jasper Makalla, wakati akizungumza na wanahabari habari jijini Dar es Salaam amesema balozi mbalimbali zilizopo nchini na mashirika ya kimataifa yanatarajia kushiriki.

"Mashirikia zaidi ya 2,000 ya hapa nchini pamoja na  wawakilishi kutoka nchi za Uganda, Ethiopia, Zambia na Malawi wanatarajiwa kushiriki katika jukwaa hili, lenye lengo la kubadilisha uzoefu na kushirikisha changamoto na masuluhisho ili kuboresha mazingira wezeshi kwa mashirika yasiyo ya Kiserikali,"amesema Makalla 

Pia, amesema kutakuwepo na huduma mbalimbali za usaidizi wa kisheria na maonesho nitakuwepo siku hiyo.

"Kutakuwa na matukio mbalimbali kama, maonesho ya kazi za mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi katika maeneo ya Nkuhungu, Chang'ombe na Chamwino,"amesema .

" Pia kutakuwa nan Semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza la NaCoNGO na wasajili wasaidizi, Mikutano ya pembeni ya kujengeana uwezo pamoja na uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza utapiamlo kwa Watoto.,” alisema Makalla.

Mwenyekiti wa Jukwaa Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO), Jasper Makalla akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini DaresSalaam, baada ya kuzungumza kuhusu jukwaa la nne la linatarajia kufanyika jijini Dodoma Septemba 4 hadi Septemba 6,2024.

Aidha, amesema baraza limeanzisha mchakato wa kupitia upya kanuni zake za muhimu ambazo zinaiwezesha Baraza kufanya majukumu yake kwa weledi Zaidi.

Amesema kuwa Tanzania Bara kuna mashirika yasiyokuwa ya kiserikali takribani 9,400 yanayofanya kazi katika mbalimbali katika kutumikia jamii ya Watanzania, hivyo wanahitaji kupitia kanuni hizo ili kuongeza uwajibikaji.

Alibainisha kuwa upitiaji kanuni hizo utafanya Baraza liweze kufanya majukumu yake ipasavyo.

"Mchakato  huo unagusa mapitio ya Kanuni mbili zinazoongoza baraza ili kuweza kuimarisha utendaji kazi wa Baraza kukuza udhibiti binafsi" amesema 

Alizitaja kanuni hizo kuwa ni Kanuni za Utendaji wa Baraza la Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali na Kanuni za Uchaguzi wa Baraza la NaCoNGo zote za mwaka 2016.

Pia, amesema kuwa  mapitio ya kanuni hizo yanalenga kuhimiza ukuaji na kuunda fursa mpya kwa NGOs, Serikali na wadau wakuu katika sekta ya NGOs.