KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu amemtaka Waziri wa kilimo Hussein Bashe na Taasisi ya Kuzuia Kupambana na Rushwa, TAKUKURU kuichunguza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA, kujua sababu ya wakulima kucheleweshewa malipo ya fedha zao.
Dorothy aliyasema hayo jana Katika mwendelezo wa ziara yao alipoongea na wananchi Katika mkutano wa hadhara Handeni mkoani Tanga.
KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu amemtaka Waziri wa kilimo Hussein Bashe na Taasisi ya Kuzuia Kupambana na Rushwa, TAKUKURU kuichunguza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA, kujua sababu ya wakulima kucheleweshewa malipo ya fedha zao.
Alisema hayo baada ya kupokea malalamiko kwa baadhi ya wananchi yakiwamo ya kutolipwa kwa wakati wanapouza mazao yao hali inayochangia kujitokeza madalali wanaowalalia kwa kununua kwa bei ndogo.
Alisema kwa ukuaji wa teknolojia katika ulimwengu wa sasa inashangaza kuona zinapita mpaka siku 14 mkulima hajalipwa fedha zake.
Alisema walitegemea NFRA, ingemsaidia mkulima apate mahali salama pa kuuza mahidi yake, bei nzuri ili afaidike na kilimo chake lakini wamepokea taarifa nyingi za wakulima wa mahidni namna wanavyo nyanyaswa.
"Tuna serikali ambayo haisikilizi shida za wananchi tumesikia bunge linapitisha bajeti, baadala ya kupunguza mzigo wa Kodi kwa wananchi limeenda kuongeza tulikuwa tunalipia Kodi ya nyumba Sh 1000 Sasa hivi ni Sh 2000 hiki ni kielelezo tosha kwamba imeshidwa kumtoa Mtanzania kwenye wimbi la umasikini.
"Ukiangalia maeneo mengi ya vijijini mambo ni yaleyake hakuna umeme, maji, shule, vituo vya afya hapa Tanga wananchi wamejitolea kujenga zahanati lakini hata kuwawekea umeme imeshindikana.
Alisema Tanga inaongoza kwa kilimo cha mahindi ikizalisha asilimia 65 akikumbushia kuwa kwa mwaka 2019-2020 ulizalisha zaidi ya tani 429.
Dorothy aliwaomba Wanatanga kujitokeza kwa wingi kuchagua viongozi wanaotokana na chama hicho akisisitiza watakuwa kipaumbele kuwawezesha kujenga uchumi imara na kuhakikisha kila Mtanzania anafanya kazi na kupata ujira stahiki.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED