Bonanza lahamasisha uandikishaji Daftari la Kudumu Wapigakura

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:44 PM Feb 23 2025
Mbunge wa Jimbo la Malindi Zanzibar, Mohammed Suleiman Omar (kulia) akisikiliza kwa makini ushauri wa kitaalamu baada ya kupimwa afya yake na mwanachuo kutoka SUZA, Irene Fabian Matiku.
Picha Zote: Martin Kabemba
Mbunge wa Jimbo la Malindi Zanzibar, Mohammed Suleiman Omar (kulia) akisikiliza kwa makini ushauri wa kitaalamu baada ya kupimwa afya yake na mwanachuo kutoka SUZA, Irene Fabian Matiku.

UMOJA wa Vijana wa CCM, Wadi ya Malindi Zanzibar, umeandaa Bonanza la mpira wa ufukweni kuhamasisha uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura, lililofanyika kwenye ufukwe, mjini Zanzibar.

Kwenye bonanza hilo matawi manne ya Jimbo la Malindi yalishiriki.

Mbunge wa jimbo la Malindi, Mohamed Suleiman Omar akiongea na wanamichezo
Mbunge wa Jimbo la Malindi, Mohammed Suleiman Omar, akikabidhi kikombe kwa nahodha wa timu ya Malindi, Haji Bakari Ali, baada ya kuifunga timu ya Kiponda mabao 8 - 2 katika mchezo uliofanyika kwenye ufukwe, mjini Zanzibar jana.

Mbunge huyo aliongea na wanamichezo, baada ya kuhitimisha bonanza la kuhamasisha uandikishaji  lililofanyika kwenye ufukwe, jana.

Mbunge wa jimbo la Malindi, Mohammed Suleiman Omar akikabidhi kikombe
Wananchi wengi walipima afya zao kwenye bonanza hilo. Pambano la mpira wa ufukweni kati ya timu ya Kiponda na timu ya Shangani (yellow) kwenye ufukwe wa hoteli ya Serena Inn mjini Zanzibar.

Kiponda iliichapa Shangani mabao 3 - 2.