BRELA yawaita wafanyabiashara kujisajili ndani ya muda mfupi

By Vitus Audax , Nipashe
Published at 05:41 PM Sep 13 2024
BRELA yawaita wafanyabiashara kujisajili ndani ya muda mfupi
Picha: Mpigapicha Wetu
BRELA yawaita wafanyabiashara kujisajili ndani ya muda mfupi

Ikiwa zimesalia siku mbili kabla ya kumalizika kwa maonesho ya 19 ya wafanyabiashara Afrika Mashariki yanaoyoendelea katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, wanyabiashara wameendelea kusajili biashara na majina ya biashara zao ili kuwa na hatimiliki binafsi.

Kadhalika Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umeendelea kuwaita wafanyabishara kuwahi fursa ya kusajiliwa na kupatiwa vyeti papo kwa papo na kuwa na umiliki halali wa biashara, kampuni pamoja na majina yake.

Kauli hiyo imetolewa jana na Ofisa Msaidizi wa Usajili BRELA, Selemani Selemani akizungumza na Nipashe wakati wa utoaji wa huduma katika banda la BRELA lililopo kwenye maonesho hayo.

“Tunapenda kuwakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Mwanza na maeneo jirani kuhudhuria katika banda letu ili kupata elimu juu ya shughuli mbalimbali ambazo tunazifanya na kusajili papo kwa papo,” alisema Selemani.

1
Aidha alisema katika huduma wanazozitoa ni pamoja na kusajili majina ya bishara, kuhuisha taarifa za biashara pamoja na kutoa elimu bora inayohusiana na biashara au kampuni.

Baadhi ya wananchi waliopata huduma za kusajili biashara zao katika maonesho hayo na kupata vyeti akiwemo Omary Said walieleza kufurahishwa na huduma hiyo inayotolewa ndani ya muda mfupi.

Naye Omary Mustapha ambaye tayari amepata cheti cha usajili wa biashara yake ya kielektroniki alieleza kutumia Sh.20,000 pekee ambayo aliilipa kwa njia ya ‘control number’ na kuchuku muda mfupi kukamilishiwa huduma hiyo.

“Niwaite vijana wenzangu wenye biashara kufika katika viwanja hivi kupata huduma kabla ya maonesho haya kutamatika kwani huduma hii inatolewa kwa haraka zaidi,”alisema Mustapha

2