Makonda asema wapo watumishi wanafiki na kujipendekeza

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 11:26 PM Apr 21 2024
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda.

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amesema kumekuwa na watendaji wengi wenye unafiki na kujipendekeza hawawezi kazi na kazi yao kubwa ni kuwasifia viongozi.

Kadhalika, Makonda amesema ana taarifa za watumishi wote ambao wanapokea rushwa kwenye utekelezaji wa majukumu yao na kuwataka mwisho wao uwe jana.

Makonda aliyasema hayo leo mkoani humo wakati akiongoza kikao kazi na taasisi za umma na mamlaka za serikali za mitaa mkoani Arusha.

“Tumekuwa na watendaji wengi wenye kasumba za unafiki na kujipendekeza tena wasioweza kazi, kazi yao kubwa ni kuwasifia viongozi ndio maana hata hapa nimemsikia MC anasema tumpigie makofi ameanza kazi. Kazi yenyewe sijaanza bado hata najifunza makofi ya nini,”amesema Makonda na kuongeza kuwa; 

“Kupambana pambana huku kumetufanya tunaishi maisha tofauti na wananchi tunaowaongoza wanatutizama tofauti na sisi viongozi tupo kwenye dunia nyingine tofauti na matokeo yake wananchi wanashindwa kujivunia viongozi wao,”.

Amesema namba moja ni lazima wakubalia hakuna sababu yoyote ya kusifiana acha kazi ziongee.