Rais wa Bukina Faso kushiriki mkutano wa nishati Dar

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:01 PM Jan 23 2025
Rais wa mpito wa Bukina Faso, Capt. Ibrahim Traoré.

Rais wa mpito wa Bukina Faso, Capt. Ibrahim Traoré ni miongoni mwa marais 25 watakaoshiriki mkutano wa nishati uliopangwa kufanyika Dar es Salaam Januari 27 na 28 mwaka huu.

Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeshughulikia masuala ya nishati na mabadiliko ya hali ya hewa, Dk.Kevin Kariuki amesema pia mawaziri wa fedha na nishati 60 wa Afrika watashiriki mkutano huo. 

Aidha, viongozi wengine wa kimataifa watashuhudia wakuu wa nchi za Afrika wakikubaliana kusaini Mpango Mahususi wa Nishati wa Afrika, awamu ya kwanza utakaozishirikisha nchi 14. Nchi hizo ni Tanzania, Malawi, Chad, Nigeria, Burkina Faso, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Niger, Liberia, Msumbiji, Madagascar, Zambia, Mali, Ivory Coast na Mauritania. 

Alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mkutano huo unadhaminiwa na Benki ya Dunia, AfDB na washirika wengine wa maendeleo kuhakikisha watu milioni 300 Afrika wanafikiwa na umeme ifikapo mwaka 2030.