Viongozi wa kijeshi wa mataifa ya Niger, Burkina Faso na Mali, wameunda kikosi cha pamoja ambacho hivi karibuni kitatumwa kwenye eneo la ukanda wa Sahel kukabiliana na makundi ya kijihadi yanayoripotiwa kuongezeka.
Waziri wa Ulinzi wa Niger Salifou Mody amesema Kikosi hiki chenye wanajeshi 5000 kimekabidhiwa vifaa vya anga, ardhi na maafisa wa ujasusi waliobobea na kwamba kitatekeleza mashambulio ya pamoja.
Katika miaka ya hivi karibuni, mataifa hayo yaliyojiondoa kwenye Jumuiya ya kiuchumi ya ECOWAS, yanasumbuliwa na wanajihadi wanaoshirikiana na Islamic State, hali ambayo imehatarisha maisha ya raia wa kawaida.
Kuundwa kwa kikosi hiki kunakuja baada ya mataifa haya kujiondoa katika muungano wa awali wa G5 Sahel, wakisema operesheni zake hazikuwa na faida kwao.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED