Prof. Mbarawa ahimiza utekelezaji uwanja wa ndege

By Hamida Kamchalla , Nipashe
Published at 02:38 PM Jan 23 2025
Prof. Mbarawa ahimiza utekelezaji uwanja wa ndege.
Picha: Mpigapicha Wetu
Prof. Mbarawa ahimiza utekelezaji uwanja wa ndege.

Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amemuagiza mkandarasi wa kiwanja cha Ndege Kigoma kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha kinakamilika kwa wakati kutokana na kuchelewa kulikosababishwa na sababu mbalimbali.

Prof. Mbarawa ameyasema hayo jana alipotembelea kwa lengo la kukagua mradi huo wa upanuzi na ukarabati wa Kiwanja cha Ndege Kigoma ikiwa ni sehemu ya mradi wa viwanja vinne ambapo viwanja vingine ni Tabora, Shinyanga na Sumbawanga vyote vikigharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 46.6.

"Wananchi wa Kigoma wamesubiri maboresho ya kiwanja hiki kwa muda mrefu hivyo tumsukume mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kazi imalizike haraka iwezekanavyo,"  alisema Mbarawa.

Pamoja na hayo Prof. Mbarawa amemuagiza mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads) kusimamia ubora katika ujenzi wa kiwanja hicho pamoja na kuharakisha uagizaji wa vifaa vya kukamilisha ujenzi wa jengo la abiria ili kutokwamisha kasi ya ujenzi huo.