RAIS wa Marekani, Donald Trump, ameonya Russia na kwamba ataiongezea ushuru na vikwazo zaidi, iwapo Rais Vladimir Putin, atashindwa kumaliza vita nchini Ukraine.
Ameandika katika mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, amesema kuwa kushinikiza kutafuta suluhu ya vita hiyo ni kuipendelea sana Russia na rais wake.
Trump awali alisema kuwa atajadili suluhisho la uvamizi kamili wa Russia, uliozinduliwa Februari, 2022, kwa siku moja.
Russia, bado haijajibu matamshi hayo, lakini maofisa waandamizi wamesema katika siku za hivi karibuni kuna fursa ndogo kwa Moscow kushughulika na utawala mpya wa Marekani.
"Suluhisha sasa na kuacha vita hivi vya kijinga! hali itakuwa mbaya zaidi. Kama hatufanyi mpango na hivi karibuni, sina chaguo jingine zaidi ya kuweka viwango vya juu vya kodi, ushuru, na vikwazo, kwa chochote kinachouzwa na Russia kwa Marekani, na nchi nyingine kadhaa zinazoshiriki.
"Acha tuache vita hivi, ambavyo visingeanza kama ningekuwa Rais, tena! Tunaweza kufanya hivyo kwa njia rahisi au njia ngumu na njia rahisi daima ni bora. ..."
BBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED