MGOMBEA wa nafasi ya uenyekiti Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), Mahmoud Ali Youssouf, amesema iwapo atachaguliwa, vipaumbele vyake ni pamoja na uwekezaji kwenye TEHAMA, ili kurahisisha upatikanaji intanetio na bei nafuu hadi vijijini, barani Afrika.
Youssouf, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na na Ushirikiano wa Kimataifa Djibouti, amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam.
Awali, akiwa jijini humo, amekutana na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amekutana na kuzungumza pamoja na Mjumbe Maalum wa Rais wa Djibouti, Ismail Omar Guelleh, Ikulu, leo.Amesema anawania nafasi hiyo pamoja na wagombea wengine kutoka nchi ya Kenya na Madagascar, Mauritius, akieleza kwamba anafaa kutokana na uzoefu wake kidiplomasia.
Ameeleza kuwa katika siku 100 ofisini atazingatia pia vipaumbele vingine ambayo ni kilimo, uchumi, afya, miundombinu, ili kuliondoa bara hilo kwenye utegemezi wa ki loluchumi.
"Nitazibadili changamoto kuwa fursa. Nina uzoefu wa kutosha kutokana na uzoefu nilionao. Niishinda nitawezesha upatikanaji wa intaneti na wa bei rahisi hadi vijijini, ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia duniani.
Umoja wa Afrika (AU), ulitoa majina ya wagombea wanne wanaowania uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC).
Wagombea walioidhinishwa ni kutoka mataifa ya Afrika ikiwa ni pamoja na Kenya, Djibouti, Mauritania na Madagascar. Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC0, zimepewa nafasi ya kutoa mrithi wa mwenyekiti wa sasa Mousa Faki, raia wa Chad, ambaye amekuwa akishikilia wadhifa huo tangu mwaka 2017.
Uchaguzi wa AUC umepangwa kufanyika Februari, 2025 wakati wa mkutano wa AU.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED