WAZIRI wa Katiba na Sheria,Damas Ndumbaro,amesema Wizara hiyo, imewekeza nguvu katika usimamizi wa mashauri ya ukatili wa kijinsia,migogoro ya wakulima na wafugaji pamoja na ya uhifadhi ili kuhakikisha kesi zinamalizika kwa wakati na haki inatendeka kwa kuwa ni maeneo ambayo yanaongoza kwa matukio mbalimbalika kwenye jamii.
Waziri Ndumbaro,alisema hayo jana jijini Arusha,wakati wa ziara yake ya kikazi,alipotembelea Ofisi ya Mashtaka ya Taifa Mkoa wa Arusha (NPS),Makao Makuu ya Polisi mkoani humo,Kituo Kikuu cha Polisi Arusha,Kituo cha Polisi Muriet na Mahabusu ya Watoto Mkoa wa Arusha.
“Katika kila sekta kuna kuwa na mambo ya kipaumbele ambayo jamii inakabiliana nayo kwa sasa mambo haya matatu ikiwamo ya uhifadhi dunia inalalamikia uharibifu wa mazingira umekuwa mkubwa na tabianchi imebadilika na majira ya mwaka yamebadilika tusiposimamiza uhifadhi na tukiruhusu wanyamapori wauawe tunakwenda kubaya hicho ni kipaumbele kwa sisi tunaohudumu kwenye sekta ya sheria na haki.
“Malalamiko ya ukatiliwa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto yamekuwa makubwa kwa kuwa kesi zimeongezeka sana na kazi ya sheria ni kutatua matatizo na tumejipanga kutumia nguvu za kisheria kupambana na hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wanaohusika katika ukamataji na kufanya upelelezi,Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Mahakama.
“Migogoro ya wakulima na wafugaji imekuwa donda ndugu imefika wakati inahatarisha amani ya nchi nalo tumeamua kulipa kipaumbele ili kuhakikisha pamoja na mambo mengi tutakayofanya lakini haya matatu yanasimamiwa kikamilifu kwa ajili ya kuyatekeleza vizuri.alisema Waziri Ndumbaro.
Hata hivyo,alisema kwa sasa NPS,wameboresha utoajia wa huduma kwa kuwa usikilizaji wa kesi hautakiwi kuvuka miaka miwili kwa kuwa nyingi zinakwisha ndani yam waka mmoja au ndani ya miezi sita.
“Huo ni utendaji ulioboreshwa sana pamoja na kiwango cha kushinda kesi hizo kimeongezeka hivyo wamejitahidi kwa kiasi kikubwa hivyo kazi yangu iliyobaki kama Waziri mwenye dhamana ni kuhakikisha wanapata rasilimali za kutosha,vitendea kazi na kuboresha maslai ya watumishi ili waweze kuongeza ufanisi wa uendeshaji wa kesi,”aliongeza Waziri Ndumbaro.
Aidha amewataka waendesha mashtaka na mawakili wa serikali kutumia ujuzi na uwezo wao kumaliza mashauri yao kwa wakati ili kama mtu ameonewa haki itendeke au kama ni wakufungwa ahukumiwe haraka kulingana na kosa alililotenda muhusika.
Naye Renatus Mkude,Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Makosa dhidi ya Binadamu na Utenga kutoka NPS, alisema Waziri Ndumbaro amefanya ziara mkoani humo,kwa ajili ya kuzitembelea taasisi zilizoko chini ya Wizara hiyo na ambazo wanashirikiana nazo kwa ngazi ya mkoa.
“Kwa mujibu wa kifungu cha 24 cha sheria ya mashtaka nchini Mkurugenzi wa Mashtaka na taasisi yake pamoja na NPS wamepewa jukumu la kuratibu upelelezi katika vyombo chunguzi, kwahiyo pia Waziri alizitembelea taasisi tunazozisimamia katika uratibu wa upelelezi ikiwamo Jeshi la Polisi,Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makoa ya Jinai Mkoa,Kituo Kikuu cha Polisi na Mahabusu ya Watoto,’alisema Mkude.
“Mheshimiwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan baada ya kuunda Tume ya Maboresho ya Taasisi za Haki Jinai walikuja na mapendekezo mapendekezo mbalimbali na moja ya pendekezo lilikuwa ni kuangali namna taasisi hizi zanafanya kazi kwa pamoja ili watu wapate haki kwa wakati' alisema Mkude
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED