De Master kuachia ngoma mpya Jumapili

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 07:53 PM Jan 24 2025
Deo Meta maarufu De Master.
Picha: Mtandao
Deo Meta maarufu De Master.

MSANII wa Mziki wa Kizazi Kipya, Deo Meta maarufu De Master amesema ameamua rasmi kurudi katika mziki baada ya kimya cha muda mrefu.

De master ambaye ni mzaliwa wa Kigoma aliyeanza mziki tangu mwaka 2002 akiwa na kundi la G Mobb na kufanikiwa kurekodi wimbo mmoja uliojulikana kwa jina la NENDA WEWE ngoma iliyofanya vizuri kipindi hicho.

Sasa tayari msaanii huyo ameingia studio na kupika chuma kingine, ambapo anataraji kuachia audio yake Jumapili inayokwenda kwa jina la KICHOMI huku video yake ikitarajiwa kutoka mwezi ujao.

“Kichomi ni ngoma ya moto sana, ninatarajia kuipandisha audio ‘youtube’ kuanzia jumapili ya kesho kutwa kwahiyo ninaomba mashabiki zangu waniunge mkono” amesema De Master