Wanasoka bora 15 wa Kiafrika wa wakati wote

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:22 AM Dec 23 2024
mwanasoka Mo Salah
Picha: Mtandao
mwanasoka Mo Salah

KWA muda mrefu Afrika imetoa baadhi ya nyota wa muda wote wa soka, ambao wengi wao wametamba na vipaji vyao barani Ulaya.

Nyota kutoka Cameroon, Nigeria na Misri, wamevutia watazamaji kote ulimwenguni, wakiandika majina yao katikati vitabu vya historia ya soka.

Wengi wa wanasoka wenye furaha barani Afrika wametundika daruga zao katika karne ya 21, lakini bado kuna idadi kubwa ya nyota ambao wanang'ara katika kiwango cha juu.

Hawa ndio wanasoka bora zaidi wa Kiafrika wa wakati wote;

15. Lauren Mayer

Lauren alikuwa mmoja wa wengi waliolelewa na Arsene Wenger na mchezaji huyo wa Kimataifa wa Cameroon alimzawadia kocha wake kwa kiwango bora kabisa. Alipowasili mwaka 2000 pale Arsenal, Lauren alikuwa muhimu kwa ushindi wote wa Arsenal wa karne ya 21 wa Ligi Kuu England, ikiwa ni pamoja na kupanga safu ya beki wa kulia wakati wa kampeni ushindi wa taji la ligi bila kupoteza.

Mshindi wa Kombe la FA akiwa na Portsmouth na bingwa mara mbili wa Kombe la Mataifa ya Afrika akiwa na Cameroon, Lauren alistaafu soka ya kimataifa akiwa na umri wa miaka 25 pekee.

14. Thomas N'Kono

Wachezaji wakuu wa Afrika mara nyingi wamekuwa wakitamba kwenye uchezaji wa ndani, lakini Thomas N'Kono alikuwa golikipa. Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Cameroon mwenye michezo 63 aliiwakilisha nchi yake kwa miongo miwili na mara nyingi alikuwa na uchezaji wa kuvutia macho katika mashindano makubwa.

Akiwa kwenye michuano ya Kombe la Dunia la FIFA mara tatu, alibeba mara mbili tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika na alitamba sana kwenye Kombe la Dunia la 1990 huku Cameroon ikifika hatua ya robo fainali. 

13. Jay-Jay Okocha

Jay-Jay Okocha alifanya mamilioni ya Wanigeria kupenda soka. Akiwa maarufu kwa ustadi wake wa chenga za maudhi, nyota huyo wa zamani wa Paris Saint-Germain na Bolton Wanderers, alicheza kwa furaha kubwa iliyowaacha watazamaji wakishangilia.

12. Pierre-Emerick Aubameyang

Pierre-Emerick Aubameyang amefifia hadi kusikojulikana kidogo katika zama za kisasa, sasa anacheza kwenye Ligi Kuu ya Saudi Arabia. Si rahisi kusahau jinsi mchezaji huyo wa Kimataifa wa Gabon alivyokuwa bora wakati wa miaka yake ya kilele akiwa Borussia Dortmund na Arsenal.

11. Nwankwo Kanu

Akiwa ameshindwa kukidhi mahitaji ya Inter Milan baada ya kuibukia Ajax, Wenger alimchukua Nwankwo Kanu pale Arsenal. Imani ya kocha huyo wa Ufaransa ilizaa matunda haraka huku Mnigeria huyo akichanua na kuwa bora kule Kaskazini mwa London.

Kanu alikuwa akivutia mara kwa mara kwani 'Washikabunduki' walishinda mataji mawili ya Ligi Kuu ya England, hata kama hakuwahi kuwa nyota wa mchezo kule Highbury.

10. Roger Milla

Roger Milla mfungaji mwenye umri mkubwa zaidi katika historia ya Kombe la Dunia (miaka 42 na 39) aliifungia Cameroon mabao manne kwenye Kombe la Dunia la 1990.

Maisha marefu ya Milla yalikuwa ya kuvutia kama vile mabao yake yanavyorejea kwa nchi yake, huku fowadi huyo akitumia muda mwingi wa maisha yake ya klabu kama mshambuliaji wa kutegemewa nchini Ufaransa.

9. Michael Essien

Michael Essien katika kilele chake alikuwa kiungo mkabaji mgumu, anayecheza mpira kwa kasi na raia huyo wa Ghana alifanikiwa kuichezea Chelsea kwa kipindi cha miaka tisa.

Bingwa huyo mara mbili wa Ligi Kuu England, mshindi mara nne wa Kombe la FA na mshindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msmu wa 2011/12, alionesha mabadiliko katika safu ya kiungo ya 'The Blues' walipochanua na kuwa nguvu kubwa duniani.

8. Riyad Mahrez

Leicester City walimsajili Riyad Mahrez kwa pauni 450,000 kutoka Le Havre mwaka 2014. Ingawa raia huyo wa Algeria alicheza vizuri katika miezi 18 ya kwanza pale kwenye Uwanja wa King Power ni msimu wa 2015/16 ambao ulimfanya ajijengee sifa kubwa zaidi.

Mshiriki muhimu wa kikosi cha Leicester kilichoshinda taji la Ligi Kuu England, winga huyo alikuwa mtoa huduma wa mara kwa mara wa Jamie Vardy na mfungaji mabao na hatimaye Manchester City wakamsajili mwaka 2018.

7. Abedi Pele

Abedi Pele hakulazimika kungoja mashindano ya kimataifa ili aonekane kwa watazamaji wa Ulaya. Raia huyo wa Ghana alijiunga na Marseille mwaka 1987 na kujitangaza kwa haraka kama mmoja wa vipaji vya ajabu sana kutoka barani Afrika.

Akiwa sehemu ya washambuliaji watatu mashuhuri wa Marseille pamoja na Chris Waddle na mshindi wa Ballon d'Or, Jean-Pierre Papin, Pele alishinda Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 1992/93.

6. Sadio Mane

Sadio Mane alitwaa ubingwa wa Ligi Kuu England akiwa na Liverpool baada ya kusajiliwa kutoka Southampton mwaka 2014. Alifunga mabao 21 katika misimu miwili ya ligi akiwa na Saints hao.

Liverpool walitumia fedha nyingi kumnunua nyota huyo wa Senegal huku kocha Jurgen Klopp akianza mapinduzi yake pale Anfield na Mane akaonekana kuwa sehemu muhimu. Winga huyo asiyechoka dimbani alikuwa mfungaji mabao aliyebobea, mpiga chenga mwenye nguvu na mchezaji wa kuvutia, akiunda safu ya wachezaji watatu wanaoheshimika zaidi enzi hizi pamoja na Roberto Firmino na Mohamed Salah.

Alishinda Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Ulaya na kumaliza wa pili katika kura ya Ballon d'Or mwaka 2022.

5. Yaya Toure

Msimu wa 2013/14, Yaya Toure alikuwa kitu kingine. Wakati Manchester City ikipambana na Liverpool ikielekea kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England, mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ivory Coast, ndiye aliyekuwa akivuta kamba na kuamua mechi.

Mabao 20 kwenye Ligi Kuu kutoka kwa kiungo wa kati si jambo la kawaida.

Toure alitwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika wa Mwaka mara nne.

4. George Weah

Mwafrika pekee aliyeshinda Ballon d'Or - ukiondoa Eusebio mzaliwa wa Msumbiji ambaye aliichezea Ureno - George Weah alikuwa mtu wa kuvutia katika miaka ya 1990. Akibeba tuzo ya hadhi ya juu zaidi ya soka mwaka 1995 akiwa anaichezea AC Milan

Raia huyo wa Liberia alishinda mataji mawili ya Serie A nchini Italia akiwa tayari amefanya vema nchini Ufaransa.

3. Didier Drogba

Iwapo uliwahi kuhitaji mchezaji ili kutoa wakati wa uhakika katika uangalizi mkali zaidi, Didier Drogba, ndiye aliyekuwa mtu wa kumpigia simu. Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ivory Coast alikuwa mwanga mkali katika kikosi cha Chelsea kilichovutia wakati wa mastaa na mwanzoni mwa miaka ya 2010, akiongoza mstari kwa mchanganyiko kamili wa nguvu na usahihi.

Drogba alifunga mabao tisa katika fainali kumi alipokuwa akiichezea 'The Blues', likiwamo bao la kusawazisha na penalti ya ushindi huku Chelsea ikishinda taji lao la kwanza kabisa la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2011/12.

Mataji manne ya Ligi Kuu na  mengi zaidi ya Kombe la FA yanapatikana kwenye kabati la kuvutia la mshambuliaji huyo, huku Drogba akipewa heshima kubwa na mashabiki wa Chelsea katika kipindi cha mafanikio zaidi ya klabu hiyo.

2. Samuel Eto'o

Samuel Eto'o alichukua njia ya ajabu kidogo hadi kwenye ustaa mkubwa. Baada ya kusajiliwa na Real Madrid mwaka 1997, raia huyo wa Cameroon alicheza kwa mkopo katika klabu kadhaa za Hispania kabla ya kuwasha moto huko Mallorca.

Barcelona ndiko sehemu alikotamba zaidi Eto'o ambako alitwaa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na matatu ya Ligi Kuu Hispania, LaLiga.

Kuhamia Inter kulizaa mafanikio zaidi na taji lingine la Ligi ya Mabingwa, huku pia akitwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Afrika mara nne.

1. Mohamed Salah

Sasa tunakuja kwa mkuu zaidi, Mohamed Salah.

Ingawa mabishano yanaweza kutolewa kwa mastaa kama Weah, Drogba na Eto'o. Salah ndiye kinara kwa ubora.

Baada ya kushindwa kufanya vizuri Chelsea, Salah alijenga upya heshima yake nchini Italia akiwa na Fiorentina na AS Roma, na kuwashawishi Liverpool kumsajili mfalme huyo wa Misri.

Bado anaendelea kucheza na bila shaka yoyote bado ana mengi mazuri ya kufanya.