MWENYEKITI BAWACHA PWANI: Naona umuhimu wa ukomo wa uongozi hapo mbeleni

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 11:25 AM Dec 23 2024
Chadema
Picha: Mtandao
Chadema

MWENYEKITI wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA), Kanda ya Pwani, Rose MoshI, amesema pamoja na haki ya kila mwanachama kumuunga mkono kiongozi ambaye wanaona anafaa ndani ya chama, hapo mbeleni kunapaswa kuwapo ukomo wa uongozi.

Amesema kwa miaka ijayo, ipo haja ya kuwapo ukomo wa uongozi ndani ya chama na katiba kuweka wazi, ili kutoa fursa kwa wanachama wengine kuonesha maono yao kiuongozi.

Rose amesema hayo leo, akihojiwa na redioni Clouds fm, kuhusu mtazamo wake binafsi wa hatua ya Freeman Mbowe, kuonesha nia ya kuwania tena nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Amesema ameungana na wanawake wengine ambao wanaona ni vyema kumuunga mkono Mbowe, kushika nafasi hiyo, kwa kuwa kwa wakati huu kulingana na mwenendo wa kisiasa nchini, Mbowe anafaa.