Trump: Putin anataka tuonane

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:52 AM Dec 23 2024
Donald Trump
Picha: Mtandao
Donald Trump

RAIS mteule wa Marekani. Donald Trump, amesema Rais wa Russia, Vladimir Putin, anahitaji kuonana nae mapema iwezekanavyo.

"Rais Putin anasema anataka kukutana nami haraka iwezekanavyo.

"Kwa hivyo itabidi tusubiri, lakini lazima tukomeshe vita hivi. Vita hivi vinatisha, vinatisha."

Rais wa Russia, Vladimir Putin (katikati)
Trump alisema katika kongamano huko Arizona. Trump, ambaye atarejea Ikulu ya White House, Januari, 2025, awali wakati wa kampeni alisema kwamba akichaguliwa kuwa rais anaweza kumaliza vita hivyo chini ya saa 24.

Hivi karibuni alikosoa uidhinishaji wa Biden kwa Ukraine kutumia silaha za masafa marefu zilizotolewa na Marekani kushambulia eneo la Russia.

BBC