WATOTO yatima wa Kituo cha kulea watoto wenye uhitaji cha Huruma kilichoko Tabata na Yoco kilichoko Kinyerezi jijini Dar es Salaam wametoa shukurani kwa watumishi wa PSSSF kundi la wakimbiaji (PSSSF RUNNERS) kwa kuwapatia misaada mbalimbali ikiwemo vyakula.
Agnes Milali, ni mtoto anayelelewa katika kituo cha Yoco kilichoko Kinyerezi, amesema misaada hiyo itawasaidia, amewashukuru watumishi wa PSSSF kwa kuwakumbuka. “Tunashukuru sana tumefurahi Mungu awabariki katika kazi zenu msaada huu wa vyakula mliotupatia utatusaidia katika maisha yetu hapa kituoni,” amesema Milali.
Naye Omar Yusuf wa kituo cha Huruma ameshukuru kwa zawadi waliyopata kutoka PSSSF, "Tunashukuru sana kwa zawadi hizi mlizotupatia ikiwemo vifaa vya shule mimi kama mwanafunzi vitanisaidia.” Walezi wa vituo hivyo Hamisa Mwinyipembe wa Kituo cha Huruma na Joseph Luzagama wameshukuru na kumuomba mwenyezi Mungu awabariki katika utekelezaji wa majukumu yao.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED