Waziri Silaa asisitiza ushirikiano CCM, Serikali kutekeleza shughuli za maendeleo

By Thobias Mwanakatwe , Nipashe
Published at 02:57 PM Oct 22 2024
Waziri Silaa asisitiza ushirikiano CCM, Serikali kutekeleza shughuli za maendeleo.
Picha:Thobias Mwanakatwe
Waziri Silaa asisitiza ushirikiano CCM, Serikali kutekeleza shughuli za maendeleo.

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Jerry Silaa,amesema ushirikiano baina ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali ni wa muhimu sana kwa kuwa ndio unasaidia kufanyika vizuri kwa shughuli za maendeleo.

Akizungimza leo Oktoba 22,2024 katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano Mkoa wa Singida ya kukangua miradi ya maendeleo amepongeza ushirikiano uliopo kati ya chama na serikali katika Mkoa wa Singida na kwamba  kunapokuwa hakuna ushirikiano muda mwingi unatumika kutatua migogoro badala ya kuwahudumia wananchi.

"Kunapokuwa hakuna ushirikiano kunapokuwa migogoro,kunapokuwa hakuna kusemezana baina ya muuza duka na mwenye duka muda mwingi utatumika katika kutatua migogoro badala ya kuwahudumia wananchi," amesema.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego amesema maendeleo makubwa yamefanyika katika mkoa huu kutokana na fedha nyingi kuletwa ambapo bajeti ya mwaka uliopita zilipangwa kuletwa Sh.bilioni 239 lakini zilizoletwa ni Sh.bilioni 241. kwa ajili ya shughuli za maendeleo.