Vijana kuongezewa umahiri ufundi magari, ushonaji

By Restuta James , Nipashe
Published at 02:27 PM Jul 10 2024
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, akizungumza baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya King's Trust International (KTI), ya Uingereza anayeshughulikia Kusini mwa Jangwa la Sahara, Andre Harrima
Picha: Mpigapicha Wetu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, akizungumza baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya King's Trust International (KTI), ya Uingereza anayeshughulikia Kusini mwa Jangwa la Sahara, Andre Harrima

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya King's Trust International (KTI), ya Uingereza anayeshughulikia Kusini mwa Jangwa la Sahara, Andre Harriman, na kujadili ushirikiano katika kuimarisha mafunzo ya ufundi.

Waziri Mkenda amesema kutokana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia, serikali inaweka mkazo kuwapatia vijana ujuzi utakaowawezesha kushiriki kikamilifu katika sekta mbalimbali za uzalishaji ikiwemo viwanda.

"Nimewaambia sisi tunataka kupitia Vyuo vya ufundi (VETA), tushirikiane nao kuimarisha ujuzi katika maeneo mawili, moja  kuimarisha ni katika eneo la (Mechatronics), tuwafundishe namna ya kuwa mafundi mahiri wa magari hasa yanayotumia vifaa vya kisasa," amesema Prof. Mkenda.

Eneo lingine kwa mujibu wa Prof. Mkenda ni ujuzi katika sekta ya nguo ikilenga ubunifu wa mavazi na ushonaji. 

1

“Kuna fursa nyingi kwa Vijana wa Kitanzania hivyo tumejipanga kuwajengea umahiri kupitia mafunzo katika vyuo vyetu vya VETA kwa kuzingatia teknolojia za kisasa ili wazalishe bidhaa zinazokidhi mahitaji ya masoko ya ndani na nje ya nchi,” amesema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya KTI, Harriman ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwekeza katika miundombinu na maboresho ya Sera ya Elimu yanayowezesha wahitimu mahiri.

Amesema KTI iko iko tayari kushirikiana na Wizara katika maeneo yalitajwa kwa kuwezesha vyuo vya VETA.

2