MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema kuwa ikiwa chombo cha habari kinaanda mdahalo wa wagombea lazima ihakikishe wako kwanye usawa kwa idadi na makundi ya kijamii.
Aidha,kama chombo kitaweka mahojiano ya simu lazima wanaopiga simu wawe wametoka vyama tofauti na kama wanatoa lugha zisizofaa waondolewe hewani.
Akiwasilisha mada kuhusu Huduma za Utangazaji za Vyama vya Siasa Novemba 12,2024, Meneja wa Huduma za Utangazaji wa TCRA, Andrew Kisaka, alisema ikiwa chombo kimeanzisha madahalo wa makatibu wakuu wa vyama wa siasa wanapaswa kuwa makini sana.
Kwamba wanaohudhuria mdahalo kama ni 40 basi kila chama kiwe nauwakilishi wa wagombea 10,waliotoka kwenye makundi tofauti tofauti kwenye jamii ikiwamo wanawake,vijana na wenye ulemavu.
Alisema mwandishi hapaswi kuonyesha anapenda chama gani,bali kila chama kipata nafasi sawa ya kusikika bila upendeleo,na kujikita kutanhaza kinachoendelea.
"Wagombea waelekezwe kuzungumzia sera zao tu,wasijikite katika kutukana chama au wagombea wengine,"alisema.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED