CHADEMA yawaka wagombea 74 kuengulia yasema wasiporudishwa haufanyiki

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 08:37 PM Nov 13 2024
Mwenyeki wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam, Henry  Kileo akiongea na baadhi ya wananchama mbele ya waandishi wa habari kushinikiza wagombea 74 walioenguliwa warejeshwe.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mwenyeki wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo akiongea na baadhi ya wananchama mbele ya waandishi wa habari kushinikiza wagombea 74 walioenguliwa warejeshwe.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Dar es Salaam kimetoa wito wa kurejeshwa kwa majina ya wagombea wake 74 walioenguliwa katika Wilaya ya Kinondoni, kikisema sababu zilizotumika kuwaondoa hazina msingi thabiti.

Aidha, chama hicho kimesisitiza kuwa iwapo majina hayo hayatarejeshwa, hakutakuwa na uchaguzi katika maeneo ambayo wagombea wake wamekatwa, na kina uwezo wa kuzuia zoezi hilo.

Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Dar es Salaam, Henry Kileo, akizungumza na vyombo vya habari leo, alisisitiza kuwa wagombea walijaza fomu kwa uangalizi wa jopo la wanasheria na kwa kuzingatia kanuni zote za uchaguzi.

Kutokana na malalamiko kutoka kwa vyama vya upinzani juu ya kuenguliwa kwa wagombea wao, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, alizielekeza kamati zote za rufani za wilaya kuwapa nafasi wagombea walioenguliwa kufanya mapitio ya maamuzi hayo ili haki itendeke kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi.

Mchengerwa alisisitiza kuwa ofisi yake itaendelea kusimamia misingi ya utawala bora ili wananchi wapate fursa ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Kwa mujibu wa Kileo, wagombea walioenguliwa tayari wamewasilisha pingamizi, ingawa hakuna hatua mpya zilizochukuliwa dhidi yao.