Prof. Janabi; 'Unatawala mlo wako, ama unakutawala'

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 06:06 PM Aug 27 2024

MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi.
Picha: Mtandao
MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi.

MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi, anasema katika kukabiliana na Magonjwa Yasiyoambukiza (NCDs), binadamu anaweza kujipa mbinu za kutawala idadi ya milo yake kwa siku, licha ya kuwapo ya milo mitatu iliyozoeleka rasmi.

Anasema kufunga ni miongoni mwa mbinu za kitaalamu, kwa kutumia hatua za upangaji wa kufunga ndani ya saa 24 na mtu anaweza kuchagua ni muda upi wa kula, au idadi ya milo kwa siku, ale mara moja au mara mbili, pungufu na idadi rasmi ya milo kwa siku.

Prof. Janabi, ambaye pia ni Mhadhiri Mshiriki wa Chuo Kikuu cha Magonjwa ya Moyo cha Marekani (FACC), anatoa darasa hilo katika kitabu chake; Mtindo wa Maisha na Afya Yako.

“Zipo aina na taratibu nyingi za kufunga kwa vipindi au saa. Kila moja inategemea afya ya mtu, sababu ya kufunga na analenga kupata nini. Wakati ukiwa na njaa kwa muda mrefu, mwili hutafuta sehemu ya kupata nishati (energy) ya kujiendesha. 

Mfano wa kufunga kwa vipindi saa (intermittent fasting). Mtu anaweza kuamua kupata kifungua kinywa saa sita mchana na chakula cha usiku saa mbili usiku. Maana yake ni kwamba mtu huyu atakuwa arnefunga saa 16 na kula saa kwa nane (l6:8).

Mtu anaweza kuamua kupata kifungua kinywa saa sita mchana na chakula cha usiku akapata saa 12 jioni. Maana yake ni kwamba mtu huyu atakuwa amefunga saa 18 na kula kwa saa sita (l8:6).

Mtu anaweza kuamua kupata kifungua kinywa saa nane mchana na chakula cha usiku saa 12 jioni. Maana yake ni kwamba mtu huyu atakuwa amefunga saa 20 na kula kwa saa nne (20:4).

Mtu akiamua kula mlo mmoja tu, maana yeke anakuwa amefunga kwa saa 23 na kula kwa saa moja (23:1),” anafafanua.

Prof. Janabi, anasema mwili unakuza kinga kwa kutumia mbinu ya kufunga, kwamba ufungaji wa muda mrefu, aghalabu wa mlo mmoja kwa siku una matokeo mengi chanya, mojawapo ikiwa ni mwili kujisafisha wenyewe (autophagy). 

“Mwili huchukua akiba iliyotunzwa kwenye ini, misuli na na tumbo kwa ajili ya kutengeneza nishati ya kuendesha mwili. Katika kuchukua kila kinachoweza kutumiwa, mwili huchukua kila kitu ikiwamo wadudu kama bakteria, virusi na kila aina ya seli haribifu na kuviondoa mwilini hivyo kuacha mwili na utimamu wa kinga. 

Hali hii inapotokea siyo tu kwamba mtu anapata faida ya kupunguza uzito, bali inaimarisha kinga na kuwa na afya madhubuti na uzito unaokubalika kulingana na vipimo vya BMI,” anasema Prof. Janabi.

Bingwa huyo wa magonjwa ya moyo, anasisitiza kwamba kadri muda wa kufunga unavyokuwa mrefu zaidi, ndivyo na hali ya mwili kujisafisha inavyokuwa kubwa na yenye ufanisi zaidi kwa kuondoa kila aina ya uchafu mwilini. 

“Hali hii ndiyo inaimnarisha kinga na kumfanya mtu awe na maisha marefu zaidi yenye afya ubora. Tafiti za kisayansi zinaonyesha kuwa ukuaji wa chembechembe zinategemea sana sukari. 

Kupunguza vyakula vyenye sukari nyingi inasaidia kujikinga na kupata saratani au kwa walionayo kupunguza au kuacha kabisa, ili kudumaza ukuaji wa saratani mwilini.

Mkusanyiko wa mafuta (cholesterol) kwa muda mrefu husababisha ugonjwa wa mishipa (atheroscierosis) arnbao unahusishwa sana na kiharusi, kisukari na mengineyo.”