Mchungaji Peter Msigwa, amesema amejiunga Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa sababu upinzani haujui unakokwenda ni sawa na chombo kilichoko angani hakijui kinakwenda kutua wapi kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ametekeleza kila kitu.
Msigwa ameyasema hayo leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mwijuma, Mwananyama Wilaya ya Kinondoni, mkoani Dar es Salaam, wakati wa ziara ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Amos Makalla.
Amesema CHADEMA kinandamana maeneo mbalimbali, lakini Mwenyekiti wake anapopanda jukwaani anakuwa hana hoja kwa sababu Rais Samia ametekeleza kila kitu kwa vitendo.
"Kwa nini tusimuunge mkono Rais Samia ana mipango yenye dira unaona unakoenda, CHADEMA ni kama chombo kilichoko angani hakijui kinakwenda kutua wapi.
Msigwa amesema njia sahihi ya kuleta mabadiliko ni kwenda na Rais Samia ambaye filamu ya Royal Tour aliyoifanya imeleta watalii wengi Tanzania.
Amesema mwenyekiti wa CHADEMA hajui muda wake wa kuondoka jukwaani.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED