NSSF yatunukiwa tuzo ya mlipakodi mzuri kwa hiari kitaifa 2023/24

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:51 PM Jan 25 2025
NSSF yatunukiwa tuzo ya mlipakodi mzuri kwa hiari kitaifa 2023/24.
Picha: Mpigapicha Wetu
NSSF yatunukiwa tuzo ya mlipakodi mzuri kwa hiari kitaifa 2023/24.

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) imetunukiwa tuzo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikiwa ni sehemu ya juhudi za TRA kuthamini mchango wa walipa kodi katika maendeleo ya Taifa.

NSSF imepata tuzo hiyo baada ya kuingia kwenye kipengele cha mlipa kodi mzuri kwa hiari Kitaifa kwa Taasisi za Umma kwa mwaka 2023/24.

 Tuzo hiyo inahusisha kiasi kikubwa cha ukusanyaji wa mapato kwa mwaka 2023/24 na Mlipakodi ambaye hajahusika katika udanganyifu wowote au ukwepaji kodi kwa kipindi kinachozingatiwa.

Hafla ya utoaji tuzo hizo ilifanyika tarehe 23 Januari, 2025 ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania. 

Katika hafla hiyo NSSF iliwakilishwa na Mkurugenzi wa Fedha Yahya Ally ambaye alipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Masha Mshomba. 

Hatua ya NSSF kupata tuzo hiyo ya Mlipakodi mzuri kwa hiari Kitaifa katika Sekta ya Taasisi za Umma ni matokeo ya NSSF kuzingatia kanuni na taratibu za ulipaji kodi kwa maendeleo ya Taifa.