Katika kuhakikisha wageni watakaohudhuria mkutano mkubwa wa nishati wanakuwa salama kiafya muda wote, Waziri wa Afya Jenister Muhagama ametembelea hospitali ya Aga Khan iliyoko Jijini Dar es Salaam kwaajili kuangalia namna walivyojipanga kupokea wagonjwa ikitokea dharula.
Mkutano huo utawakutanisha Wakuu wa Nchi 53 wa Afrika wanaojihusiha na masuala ya nishati unaotarajiwa kufanyika kuanzia kesho na keshokutwa .
Akiwa Katika hospital hiyo, ambayo ni moja ya zilizopendekezwa na serikali kutoa huduma aliwataka wahudumu wake kujiweka tayari endapo itatokea dharula kwa wageni hao.
"Nchi itapokea wageni wengi kutoka Taasisi za kimataifa zinazojihusisha na masuala haya ya nishati. Ili kufanya mkutano kuwa salama kazi yetu kama Wizara ni kuzitayarisha taasisi za tiba kujiandaa kutoa matibabu kwa jambo lolote litakalotokea kipindi hiki.
"Leo nikiwa nimeambatana na katibu mkuu wangu na viongozi mbalimbali tumekagua hospital ya Aga Khan wako tayari na wamejiandaa kwa viwango vya hali ya juu.
"Kila kinachotakiwa kipo, chumba Cha uangalizi maalumu kipo tayari kwa huduma. na mambo mengine yapo vizuri" amesifu Muhagama
Amesema pia watatumia mkutano huo kutangazwa tiba utalii ndani ya nchi, na kwamba ni nafasi nyingine kwa taifa kutangaza uwezo wa kutoa matibabu ya kibingwa na kibobevu.
Mganga Mkuu wa Taasisi ya Afya Aga Khan Tanzania, Harrison Chuwa, ameishukuru serikali kwa kuichagua hospitali yao kuwa miongoni mwa zitakazotoa huduma kwa wageni ikitokea dharula.
"Tumempitisha katika vitengo vyetu vyote muhimu waziri na timu yake ya wameridhika na maandalizi tuliyoyafanya" amesema Chuwa
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED