MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ametangaza kuongoza operesheni maalum ya siku tatu ya kurejesha haki kwa wananchi.
Makonda ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha, kuwa oparesheni hiyo itaanza Mei 8 hadi 10 mwaka huu na itajulikana ni wiki ya haki kila mmoja atarejeshewa haki yake.
“Kama ni suala la haki za watoto, ukatili wa kijinsia kama ni sekta ya ardhi umekosa haki yako iwe ni biashara ama kuna jambo ambalo uliunianza na mtu ukampatia kila kitu matokeo yake katumia ubabe wake kukunyima haki yako njoo nitasimama katika nafasi yangu,”
Amesema atabaki kuwa sauti ya wananchi wake anapokea kilio cha watu wasiosikika, hivyo amewaomba wajitokeze kupatiwa haki zao.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED