DED Mkalama asisitiza wananchi kushiriki Uchaguzi Serikali za Mitaa

By Thobias Mwanakatwe , Nipashe
Published at 10:42 AM Aug 27 2024
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Messos
Picha: Mpigapicha Wetu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Messos

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Messos, amewataka wananchi wilayani humo kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 2024.

Ametoa wito huo  jana wakati wa ziara ya kikazi ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa vijiji vya Gumanga na Nduguti wilayani hapa

“Nawasihi msipoteze haki zenu za msingi, utakapofika wakati wa kujiandikisha, mjiandikishe, utakapofika wakati wa kampeni jitokeze na itakapofika wakati wa kupiga kura tujitokeze kuwachagua viongozi wetu tunaowataka,” alisema.

Akizungumzia suala la maadili, Messos amewakumbusha wakazi wa vijiji vya Nduguti na Gumanga kuwa mstari wa mbele kupinga mila na desturi zinachochea mmomonyoko wa maadili katika jamii.