SERIKALI imetenga zaidi ya Sh. trilioni moja kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa meli katika Ziwa Tanyanyika na Ziwa Victoria ili kuwezesha huduma ya usafiri na usafirishaji kuwa bora katika maziwa hayo.
Hivyo, imehamamisha wawekezaji wa sekta ya usafiri na usafirishaji kuendelea kuwekeza Tanzania kutokana na amani na mazingira wezeshi ya uwekezaji yaliyoko.
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile, aliyasema hayo mkoani Dar es Salaam, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa magari ya Kampuni ya Foton kutoka nchini China.
“Serikali imeendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ya uchukuzi ili kurahisha usafirishaji mizigo na abiria wa ndani na nje ya nchi, hivyo ujio wa kampuni hii ya Foton utasaidia kukuza sekta hii ya usafirishaji,” alisema Kihenzile.
Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Hanif Salamha alisema kwa sasa wamefungua ofisi katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Angola na Msumbuji, hivyo kufanya huduma hiyo kuwa bora kwa watumiaji.
Hanifa alisema kwa Tanzania wanategemea kufungua ofisi katika mikoa ya Dar es Salaam, Mafinga, Songea, Babati, Majimoto na Kahama.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED