TAMISEMI-Kama huna shughuli halali ya kuingiza kipato uwezi kugombea

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:06 PM Nov 12 2024
Ofisa wa Sheria wa TAMISEMI, Mihayo Andrew.
Picha:Nipashe Digital
Ofisa wa Sheria wa TAMISEMI, Mihayo Andrew.

WIZARA ya TAMISEMI imesema moja ya sharti la wagombea ni kuwa na kanuni za uchaguzi ni kuwa na shughuli halali ya kumwezesha kuingiza kipato.

Ofisa wa Sheria wa TAMISEMI, Mihayo Andrew ameyasema hayo leo Novemba 12,2024, wakati akizungumza na wahariri kuhusu kanuni na sheria za uchaguzi wa serikali za mitaa.

Aidha,amesema hakuna tafsiri ya shughuli halali,lakini kwa akili ya kawaida ni yeyote ambayo inafanyika kwa mazingira halali na kumpa mtu kipato halali.

"Anapata kipato cha kukidhi mahitaji yake,zinatambulika na mamlaka kisheria,na kwamba ujasiriamali ni shughuli inayotambulika kisheria,"amesema.

Aidha, Mkude amesema kwa yeyote ambaye alijaza ujasiriamali na jina lake likakatwa anapaswa kukata rufaa kwa kamati husika. 

"Tangu kubandikwa kwa wateule vyama vya upinzani vimelalamikia wagombea wao kukatwa bila sababu za kueleweka,na wachache waliobakia waliwekewa pingamizi na wagombea wa vyama vingine walioshinda,"amesema.

Amesema sifa za mgombea ni awe na mtaji yeyote kwenye kijiji au mtaa wake,awe Rais wa Tanzania,awe na Umri wa miaka 21,ajue kusoma,kuandika lugha ya kiingereza na kiswahili,na adhaminiwe na chama chake cha siasa.

Aidha,amesema ikiwa mgombea hakujiandikisha kwenye Daftari la Wakazi pia anapoteza sifa za kugombea kwa kuwa anapaswa kuwa mfano kwa wengine.