HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH), inatarajia kuanzisha huduma mpya kwa wenye uzito kupindukia, kwa kuudhiti unene kwa kusitisha mfumo wa mshipa wa fahamu unaosababisha hamu ya kula mara kwa mara.
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Mohamed Janabi, akizungumza na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam, akizungumza na waandishi wa habari, akisema atakayetibiwa baada ya miezi sita ataweza kupunguza kilo 12.
Amesema kwamba huduma hiyo inayotarajiwa kuanza mwakani, watashirikiana na Profesa David Prologo kutoka hospitali ya Emory Johns Creek nchini Marekani, bingwa katika tiba aina hiyo.
“Mshipa wa fahamu namba 10 ukiuzuia unakupunguzia hamu ya kula, inawasaidia wenye uzito uliopindukia. Muhimbili tunapenda kuja na tiba kubwa na mpya kila siku, kutokana na hadhi yake kitaifa.”
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED