SERIKALI imetenga zaidi ya trilioni moja kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Meli katika ziwa Tanyanyika na Ziwa Victoria ili kuwezesha huduma ya usafiri na usafirishaji kuwa bora katika maziwa hayo.
Hayo yamesemwa jiiiji Dar es Salaam na Naibu wa Uchukuzi Davidi Kihenzile wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa magari ya kampuni ya Foton kutoka China.
“Serikali imeendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ya uchukuzi ili kurahisha usafirishaji mizigo na abiria wa ndani na nje ya nchi hivyo ujio wa kampuni hii ya Foton itasidia sana kukuza sekta hii ya usafirishaji” Alisema Kihenzile.
Pia Naibu Waziri Kihenzile ametoa wito wawekezaji wa Sekta ya Usafiri na Usafirishaji kuendelea kuwekeza Tanzania kutokana na amani na Mazingira wezeshi ya uwekezaji yaliyowekwa na Serikali ya awamu ya Sita.
Kwa upande wake Mkuu wa Masoko wa Kampuni Foton Hanif Salamha amesema kuwa kwa sasa wamefungua ofisi katika nchi za Tanzania, Kenya,Uganda , Angola na Mozambique hivyo kufanya huduma hiyo kuwa bora kwa watumiaji.
Aidha, Hanifa amesema kuwa kwa Tanzania wanategemea kufungua ofisi katika mikoa ya Dar es Salaam, Mafinga, Songea, Babati, Majimoto na Kahama.
Kampuni ya Foton imetambulisha Magari yenye uwezo kubeba kuanzia tani kumi mpaka tani 1.9.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED